2559; Kuchimba shimo ili kujiandaa kutokuchimba shimo.
Fikiria mtu ambaye tayari yupo kwenye shimo, ambaye anataka kuondoka kwenye shimo hilo, ila bado hajawa tayari kuondoka.
Hivyo wakati anajiandaa kuondoka kwenye shimo hilo, anakuwa anaendelea kulichimba.
Nadhani wewe mwenyewe umeona mkanganyiko uliopo hapo. Iweje mtu anayetaka kutoka kwenye shimo aendelee kulichimba katika maandalizi ya kuondoka kwenye shimo hilo?
Tuachane na mashimo na tuje kwenye uhalisia.
Mara ngapi umeendelea kukopa wakati unajua kabisa unapaswa kuondoka kwenye madeni?
Mara ngapi umeendelea kupoteza muda huku ukijiambia huna muda wa kutosha?
Mara ngapi umeendelea kuharibu vitu, au kuviacha viendelee kuharibika kwa kujiambia hujawa tayari?
Mara zote unapojiambia hujawa tayari kufanya kitu, maana yake umekubali kitu hicho kiendelee kuharibika.
Kama kweli upo makini na kubadili kitu, unapaswa kuchukua hatua mara moja, iwe upo tayari au la.
Kadiri unavyochelewa kuanza, ndivyo unavyotoa nafasi kwa mambo kuendelea kuwa vibaya zaidi.
Hatua ya kuchukua;
Chochote unachojua ni muhimu wewe kufanya lakini unajiambia hujawa tayari kulifanya jua unajichelewesha.
Anza kuchukua hatua mara moja kwa pale uliopo na namna ulivyo, hupaswi kuendelea kusubiri tena.
Tafakari;
Unapojikuta kwenye simu, hatua ya kwanza ni kuacha kuendelea kuchimba. Acha mara moja na kuanzia hapo jenga kitu mbadala. Kuendelea kuchimba ni kuzidi kujipoteza, haijalishi una nia nzuri kiasi gani. Acha mara moja.
Kocha.
Asante Sana kocha.
LikeLike
Karibu.
LikeLike