2563; Warahisishie.
Jukumu kubwa kabisa na ambalo kila mmoja wetu analo kwenye kazi au biashara anayofanya ni kuwarahisishia wale ambao anawalenga.
Kwa wale ambao kazi au biashara yako inawalenga, wanachotafuta ni urahisi zaidi.
Kuna matokeo ambayo wanayataka na wanataka kuyapata kwa urahisi.
Inaweza kuwa urahisi kwenye bei, urahisi kwenye kutumia au urahisi kwenye kupata matokeo.
Watu wapo tayari kuchagua kilicho rahisi kuliko kigumu.
Hivyo wajibu wako mkubwa ni kurahisisha ili kuwapata walio wengi.
Hatua ya kuchukua;
Kila wakati fikiria na chukua hatua za kurahisisha kile unachofanya au unachouza. Hakikisha unaowalenga wanaweza kupata matokeo kwa hatua rahisi tu. Urahisi ndiyo utakutofautisha na wengine na kuwafanya watu kuja kwako.
Ila kuwa makini sana na urahisi wa bei, kila mtu anaweza kuutumia na unaweza kuwaleta wasio sahihi kwako.
Tafakari;
Katika hali ya kawaida, kuliwa na njia rahisi na njia ngumu mbele ya mtu, mara zote atachagua njia rahisi. Sasa wewe usibishane na watu kwenye machaguo yao, wape kile wanachotaka ili nao wakupe unachotaka.
Kocha.