#SheriaYaLeo (75/366); Ipe kazi yako maisha.

Kila unachofanya, kina aina yake ya kipekee ya maisha.
Pale unapokifanya kitu hicho kwa kina na kuweka umakini kwenye mambo madogo madogo ndiyo unaipa kazi hiyo maisha.

Unaifanya kazi hiyo iweze kusimama na kujitofautisha na kazi nyingine za aina hiyo.
Na pia unaifanya kazi hiyo kuweza kuwa na manufaa ya muda mrefu.

Watu wengi wanafanya kazi zao kwa kuharakisha, kwa kugusa juu juu tu na kutaka matokeo ya haraka.
Matokeo yake wanazalisha kazi zisizo na maisha, kazi za kawaida ambazo hazina cha kuzitofautisha na kazi nyingine. Hilo linapelekea kazi hizo zisidumu.

Huwezi kufikia ubobezi wa hali ya juu na mafanikio makubwa kama unafanya kazi zako kwa juu juu na kwa haraka.
Ni lazima uwekeze kwa kina kwenye kujifunza na kufanya kwa utofauti mkubwa.

Juhudi kubwa unazoweka zinaipa kazi maisha marefu na wewe kufikia ubobezi na mafanikio makubwa.

Sheria ya leo; Ione kazi yako kama kiumbe hai. Wajibu wako ni kuipa kazi yako maisha kwa namna ambayo itagusa maisha ya wengine.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji