#SheriaYaLeo (78/366); Nguvu ya matakwa na maamuzi.

Pale unapokitaka kitu kweli na unapokuwa huna mbadala mwingine wa kitu hicho, huwa unapata nguvu ya kupambana mpaka kukipata.
Unajitoa kwa kila namna na unafanya kazi kwa muda wa ziada ili upate kile unachotaka.

Pale unapojua kwa hakika nini unachotaka na unapoamua kwamba unakitaka kweli, utafanya kila namna ili kupata hicho unachotaka.

Watu wengine wanapokuangalia kwa namna unavyofanya wanaweza kuona kama una nguvu zisizo za kawaida.
Wanaweza kudhani wewe siyo mtu wa kawaida.
Lakini wasichojua ni kinachokutofautisha wewe na wao ni matakwa yako makubwa na maamuzi yako kwamba lazima upate unachotaka, maana huna namna nyingine.

Jua kwa hakika kile unachotaka, amua kwamba utakipata na jitoe kwa kila namna mpaka uhakikishe umekipata. Usikubali chochote kikukwamishe kwenye kile unachotaka.

Sheria ya leo; Kupanda na kufikia ngazi ya juu kabisa ya ubobezi inakutaka ujitoe kweli kweli. Ni lazima utake sana kile unachotaka na uamue na kujitoa kwa kila namna mpaka uweze kupata unachotaka.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji