#SheriaYaLeo (79/366); Mazoea yanayoua ubunifu.
Kikwazo kikubwa kabisa cha ubunifu kwa watu ni mazoea.
Kwenye kila tasnia, ugunduzi mpya unapopatikana na kuwa na mafanikio, huo ndiyo huchukuliwa na kuzoewa na kila mtu.
Hiyo inachukuliwa kama ndiyo njia kuu ya kufanya kitu hicho.
Kila mtu anaifuata hiyo kwa sababu ndiyo iliyozoeleka na inayoleta matokeo ya uhakika.
Lakini mazoea hayo yanaua ububifu, kwani watu hawafikiri njia mpya za kufanya kitu.
Watu hawahoji na kudadisi, wanafuata tu mazoea yaliyopo.
Ili kufikia ubobezi wa juu na mafanikio makubwa, lazima ukwepe hilo.
Lazima uendelee kuwa mbunifu na kuachana kabisa na mazoea.
Lazima uendelee kujisikiliza wewe mwenyewe na kufuata msukumo wa ndani na kuacha tu kuiga na kufuata mkumbo.
Sheria ya leo; Watu wanapenda sana vitu vipya vinavyoenda na wakati na siyo mazoea ya zamani. Kwa kutengeneza kitu kipya, utatengeneza hadhira yako mpya na kuweza kupata nguvu na mamlaka kupitia kitu hicho.
#NidhamuUafilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji