#SheriaYaLeo (81/366); Mbobezi wa ulimwengu.

Wanaofikia ubobezi wa hali ya juu siyo wale wanaojua tu kuhusu eneo walilochagua, bali wale wanaojua na maeneo mengine pia.

Ni wale wanaotafuta muunganiko uliopo kwenye maeneo tofauti tofauti na kutumia muunganiko huo kufanya makubwa zaidi.

Akili ya mbobezi wa ulimwengu huwa inaendelea kukua kadiri anavyokwenda, kwa sababu anaendelea kujifunza mambo mengi mapya.
Asili ina mambo mengi hivyo akili ya mbobezi wa ulimwengu inakazana kuwa na mengi kama asili.

Teknolojia inarahisisha sana zoezi hili la kujifunza kwa mapana na kuleta muunganiko kwenye mambo mbalimbali.
Tumia fursa hiyo kujifunza ili uweze kuona na kutumia fursa nyingi zaidi.

Sheria ya leo; Tanua ujuzi na maarifa yako kwa kujifunza kwa upana zaidi ili uweze kutengeneza muunganiko utakaokupa fursa nyingi zaidi.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji