#SheriaYaLeo (86/366); Angalia kinachokosekana.
Ni kawaida yetu binadamu kuangalia kile kilichopo na kisha kufikiri kwa namna hiyo.
Kwa kutumia kilichopo ndiyo tunafanya maamuzi mbalimbali.
Lakini kuna taarifa nyingi kwenye yale yanayokosekana.
Kuna vitu ambavyo vilitakiwa viwepo ila havipo.
Kwa kuanza kuvofikiria vitu hivyo, tunaweza kuja na ubunifu wa kipekee.
Kwenye kila unachofanya au kila hali unayokutana nayo, usiangalie tu nini kipo au nini kimetokea.
Bali pia angalia nini hakipo au nini halijatokea.
Kuna mengi utayapata kwa kuangalia kinachokosekana au ambacho hakikutokea.
Hili pia linaweza kutusaidia kuepuka utapeli au kutatua matatizo mbalimbali.
Watu wanapotaka kulaghai, kuna vitu vinavyoibua tamaa wanavyokuonyesha, ukiangalia hivyo tu umekwisha.
Ila unapoamua kuangalia nini kinakosekana kwenye maelezo unayopewa, utaweza kugundua kwa urahisi kabisa kama ni uongo au utapeli.
Sheria ya leo; Kwa kila jambo usiangalie tu kile kilichopo, angalia pia kile kinachokosekana. Jiulize nini kingepaswa kuwepo ila hakipo. Hilo litakuwezesha kuona vitu kwa namna ya tofauti na kuweza kuja na ubunifu wa kipekee.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji