#SheriaYaLeo (98/366); Usiwe mkosoaji na mkatishaji tamaa.
Kwa wale unaoshirikiana nao, onyesha kukubali kazi zao.
Usiwe mtu wa kukosoa na kuwakatisha tamaa wengine kwenye kila kitu.
Kwani hilo litakujengea sifa mbaya na wengi watakuwa wanakukwepa.
Hilo litaathiri ushirikiano wako na wengine na kuathiri kazi zako pia.
Kadiri unavyokuwa mkosoaji na mkatishaji tamaa, watu ndivyo wanavyokuficha mambo yao na hata kukupuuza kwenye yale ya msingi.
Lakini unapoonyesha kukubali kazi za wengine kwa kuwasifia na kuwatia moyo, nao pia wanafuatilia na kukubali kazi zako.
Unapowajali wengine nao pia wanakujali na ushirikiano unakuwa mzuri.
Ni ushirikiano huo ndiyo unaokupa fursa nzuri na nyingi.
Sheria ya leo; Uwezo wa kukubali kazi za wengine, kuwasifia na kuwatia moyo ni ujuzi unaohitaji sana ili uweze kujenga ushirikiano mzuri na wengine na uweze kufanya makubwa. Jijengee uwezo huo.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji