#SheriaYaLeo (101/366); Usiongee sana.

Unapotaka kuwashawishi watu kwa kutumia maneno, kadiri unavyoongea sana ndiyo unavyoonekana wa kawaida na kukosa udhibiti.

Kadiri unavyoongea sana ndivyo unavyojiweka kwenye hatari ya kuongea kitu cha kijinga.

Pia kwa kuongea sana watu wanakuzoea na kuona ni mtu wa maneno tu.
Kwa kuongea sana unatabirika kirahisi.

Makosa na matatizo mengi unayatengeneza kwa kuongea sana kuliko kwa kukaa kimya na kuongea pale tu inapokuwa na umuhimu.

Watu wote wenye mamlaka na wanaoheshimika siyo watu wa kuongea sana.
Wanaongea kwa uchache na pale tu inapokuwa muhimu kufanya hivyo.

Hilo linawafanya waheshimike na watu kusikiliza kwa makini kile wanachosema.
Kwa sababu watu wanajua siyo waongeaji sana, hivyo pale wanapoongea basi ni jambo muhimu na hapo wanampa umakini mkubwa.

Sheria ya leo; kwa kutokuongea sana unatengeneza mwonekano wa mamlaka na kuheshimika. Unapoacha kuongea sana unapunguza hatari ya kusema mambo ya kijinga.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UdadisiUpekeeUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji