2601; Nia njema.
Maovu mengi huwa yanaanza na nia njema, ambayo inawahadaa watu wasione uhalisia mpaka mambo yanapokuja kuwa mabaya.
Makosa mengi huwa yanatokana na nia njema inayowafanya watu wapuuze taratibu mbalimbali na hivyo kuzalisha makosa hayo.
Nia njema ni nzuri, lakini kwa tabia yetu sisi binadamu kama viumbe wa hisia, huwa na madhara makubwa.
Waliotutangulia walijua hilo ndiyo maana wakaweka sheria na taratibu mbalimbali.
Yote hayo ni kutulinda sisi wenyewe na nia njema zetu na za wengine pia.
Hatua ya kuchukua;
Kwenye kila eneo la maisha yako jiwekee sheria na taratibu utakazokuwa unatumia kufanya maamuzi mbalimbali ili uyafanye kwa usahihi.
Haijalishi una nia njema kiasi gani, kama maamuzi yanakwenda kinyume na sheria na taratibu zako, siyo sahihi.
Tafakari;
Ni watu wachache sana wanaofanya makosa au uovu kwa kusudia. Wengi huanza na nia njema kabisa ambayo huishia kwenda kinyume na sheria na taratibu zilizopo na hatimaye kuzalisha makosa na mauvu.
Kocha.