#SheriaYaLeo (106/366); Tengeneza wafuasi wanaokukubali.

Kwenye safari ya mafanikio unawahitaji watu.
Unahitaji kuwa kiongozi ambaye una wafuasi wanaokukubali.
Wafuasi ambao wanaendana na maono makubwa uliyonayo na ambao wapo tayari kuyasimamia na kuyapambania.

Uzuri ni kwamba, kiongozi hahitaji kuwashawishi wafuasi.
Wafuasi tayari wapo, wanachotafuta ni kiongozi wa kuambatana naye.
Hivyo unapoyaweka maono yako wazi kama kiongozi, wale wanaoendana nayo wanaambatana na wewe.

Ni tabia yetu binadamu kupenda kuamini kwenye kitu kikubwa kuliko sisi.
Hivyo kiongozi mwenye maono makubwa anayoyaamini, anawavutia wengine nao kuyaamini pia.

Hii ni kuanzia kwenye familia, kazi, biashara na eneo lolote ambalo kuna watu. Kuwa kiongozi mwenye wafuasi wanaokukubali na kuamini kwenye maono uliyonayo ni hitaji muhimu kwa mafanikio yako.

Sheria ya leo; Watu wana hitaji kubwa la kuamini kwenye kitu kikubwa kuliko wao. Kuwa na maono makubwa unayoyaamini na utawavuta wengine kuyaamini pia.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji