#SheriaYaLeo (113/366); Panda mbegu za mashaka.
Mashaka ni silaha yenye nguvu kubwa unayoweza kuitumia kumkabili adui.
Unapovuruga sifa yake kwa kufanya watu wamtilie mashaka, anabaki na jukumu kubwa la kutunza sifa yake.
Atajikuta njia panda katika kulikabili hilo.
Akiamua kujitetea ili kuondoa mashaka hayo, bado kuna watu hawatamwamini.
Wataona katika kujitetea kwake kuna mambo anaficha.
Akiamua kupuuza na kutokujitetea atafanya watu waamini ukimya wake ni kwa wababu yale yanayosemwa ni kweli.
Kwa adui yeyote anayekusumbua, tafuta njia ya kuibua mashaka juu yake na utakuwa umemvuruga na kumwacha akihangaika kulinda sifa yake.
Silaha hii ikitumika kwa usahihi na umakini huwa ina matokeo makubwa ya kuvunja kabisa nguvu za adui ambazo huwa zinatokana na sifa anayokuwa amejijengea.
Sheria ya leo; Panda mbegu za mashaka zitakazowavuruga kabisa maadui ili uwaache wakipambana kulinda sifa zao.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji