#SheriaYaLeo (122/366); Kila mtu yupo kwenye mchezo.
Kwenye safari ya maisha, kila mmoja yupo kwenye mchezo wa madaraka.
Kuna kitu kila mtu anapigania kukipata.
Iwe ni fedha, mafanikio, utajiri, madaraka, umaarufu na mengine.
Lakini sasa, watu wamegawanyika katika makundi matatu.
Kundi la kwanza ni wanaojifanya hawapo kwenye mchezo. Hapa kuna ambao wamekata tamaa kabisa na ambao hawataki kuonekana wapo kwenye mchezo.
Kundi la pili ni wale ambao wanacheza rafu. Hawa wanatumia kila mbinu, iwe ni sahihi au siyo sahihi ili tu kupata kile wanachotaka.
Hawajali kingine chochote ila kupata wanachotaka.
Kucheza kwao rafu huwa kunawapa wanachotaka, lakini pia kunawafikisha kwenye vikwazo vikubwa.
Kundi la tatu ni wale wanaocheza kistaarabu. Hawa wanacheza mchezo kwa kuzingatia kanuni zote muhimu ili kupata wanachotaka. Wanatumia njia zilizo sahihi kupata matokeo wanayotaka.
Katika makundi haya matatu, kundi la kwanza ndiyo la kuwa nalo makini sana.
Kwani kuna watu hujificha hapo, wakijifanya hawapo kwenye mchezo kumbe hiyo ndiyo mbinu yao ya kuwahadaa wengine.
Hao ndiyo wanaoweza kukuponza na kukuangusha ili wapate kile wanachotaka.
Unahitaji umakini mkubwa kuwajua na kuhakikisha hawawi kikwazo kwako.
Na hata kwa wale ambao wanaonekana hawapo kwenye mchezo na wamejikatia tamaa, bado pia uwepo wao ni kikwazo kwako katika kucheza mchezo wako.
Hivyo lazima uwe na njia ya kuwavuka na kuwazuia wasiwe kikwazo.
Sheria ya leo; Dunia ni kama uwanja mkubwa wa michezo ambapo wote tumenasa ndani yake. Kila mmoja yupo kwenye mchezo na hakuna namna ya kuweza kukwepa mchezo mkuu wa madaraka.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji