2623; Gharama zilipojificha.
Kipo kichekesho kinaeleza mgahawa ambao ulitumia mbinu ya masoko kuwashawishi wateja kununua kwa wingi.
Mgahawa huo uliweka tangazo kwa nje likieleza; kula leo watalipa wajukuu wako.
Watu walivutiwa na hilo na kuingia kuagiza chakula.
Baada ya kula wahudumu waliwaletea bili.
Hapo ndipo wateja wakawa wanagoma kwamba tangazo linaeleza wanakula leo ila bili wanakuja kulipa wajukuu.
Na hapo wahudumu waliwaeleza kwa unyenyekevu; hii siyo bili yako, ni bili ya bibi/babu yako, hivyo unapaswa kuilipa.
Hicho ni kichekesho lakini kimebeba ukweli mkubwa kuhusu maisha.
Kila kitu kina gharama.
Kama umejutana na kitu ambacho kinaonekana kutokuwa na gharama, usikikimbilie tu, badala yake angalia wapi gharama zimejificha.
Hilo litakuepusha kuingia kwenye gharama kubwa bila ya kujua.
Unapoambiwa kitu ni rahisi au bure, jua kuna namna unakilipia bila ya wewe mwenyewe kujua.
Hatua ya kuchukua;
Kwa kila unachojihusisha nacho, jua gharama yake halisi na uwe tayari kuilipa.
Kadiri unavyokwepa na kuchelewa kulipa gharama, ndivyo unavyokuja kulipa gharama kubwa zaidi.
Lipa gharama yako mapema na ilipe kwa ukamilifu ili uweze kupata kile unachotaka.
Tafakari;
Kila chenye thamani kina gharama.
Kama gharama hiyo haionekani wazi basi jua imejificha.
Ni wajibu wako kutafuta gharama ilipojificha na kuilipa ili kupata unachotaka.
Kocha.
Kweli kabisa kocha, wajibu wangu ni kujua kwa hakika wapi gharama ilipo ili niilipe kwa wakati. Asante Sana kwa makala ya leo.
LikeLike
Karibu
LikeLike