#SheriaYaLeo (129/366); Angalia mapito yao.
Kiashiria kizuri cha tabia za watu ni mapito yao.
Kwa kuangalia historia zao na yale ambayo wamefanya huko nyuma, unaweza kupata picha ni watu wa aina gani.
Watu wanaweza kusema wamejifunza na kubadilika kutokana na yale waliyopitia, lakini siyo rahisi hivyo.
Kuna tabia huwa zinaendelea kujirudia kwa watu, hasa wanapokuwa wanapitia hali isiyo ya kawaida.
Usipuuze tabia zozote ambazo mtu amekuwa akionyesha huko nyuma.
Mfano kupotea pale anapokabiliwa na msongo, kushindwa kutimiza alichoahidi, kushindwa kwenye mahusiano mengi, kufanya kazi maeneo mengi tofauti tofauti n.k.
Vyote hivyo ni viashiria vya tabia halisi ya mtu ambayo siyo rahisi kuwajibika.
Mtu anaweza kuongea mengi mazuri, hasa pale mambo yanapokuwa sawa. Ila mambo yanapokuwa magumu, ndipo tabia yake halisi inajidhihirisha.
Zijue tabia halisi za watu kwa kuangalia mapito yao kisha fanya maamuzi sahihi kwa tabia hizo na siyo kwa maelezo au maigizo wanayokufanyia ili kukushawishi.
Sheria ya leo; Unapochagua watu wa kufanya nao kazi au kushirikiana nao, usihadaike na kile wanachokuambia au kukuonyesha sasa. Badala yake jifunze kuangalia tabia zao za nyuma, angalia mapito yao yote na wajue kwa undani kabisa. Hapo ndiyo unaweza kuwajua ni watu wa aina gani, maana tabia halisi za watu hazibadiliki haraka.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji