#SheriaYaLeo (130/366); Tambua mlipuko wa kihisia.
Pale mtu anapopata mlipuko mkali wa kihisia dhidi yako, mfano hasira ambayo haiendani na kile ulichofanya, tambua ni mbinu ya kutaka kukutawala kihisia.
Wapo watu ambao hutumia mlipuko wa hisia kuibua hisia kali ndani yako ili waweze kukutawala.
Wanajua ukishakuwa na hisia kali, huwezi kufikiri vizuri na hivyo utafanya maamuzi yasiyo sahihi.
Usikubali kubeba hatia ya hisia alizonazo mtu.
Wengi hukusanya hisia hizo kwa muda mrefu, kutokana na yale waliyopitia kwenye maisha yako.
Hivyo wanapokuja kutoa hisia hizo kwako, usinase kwenye mtego wao, jua ni mbinu wanayotumia kutaka kukuadhibu au kukutawala.
Usikubali mtu yeyote aibue hisia kali ndani yako, hata kama ana mlipuko mkali kiasi gani wa hisia.
Dumisha utulivu wa ndani ili uweze kuona kila kitu jinsi kilivyo na kufanya maamuzi sahihi.
Sheria ya leo; Pale wengine wanapolipuka kwa hisia kali, usinase kwenye mtego wao, badala yake tumia hilo kwa manufaa yako. Tuliza kichwa chako wakati wao wanapoteza mioyo yao. Usikubali yeyote akutawale kupitia mlipuko wa hisia. Utulivu wa ndani ni silaha kubwa na muhimu kwako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji