2632; Unachojali zaidi.
Kila unachokijali zaidi kwenye maisha yako ndiyo kinapata kipaumbele kikubwa kwako.
Hicho kitakuwa na nguvu ya kukusukuma ufanye au usifanye mambo muhimu unayopaswa kufanya.
Chukua mfano unataka kupata fedha ili kufikia uhuru wa kifedha, lakini pia unataka kila mtu akupende.
Kitendo cha kujali kuhusu kupendwa na kila mtu kinakuwa kikwazo kwako kupata fedha unazotaka.
Kwa maneno mengine ni kwamba kama kuna kitu kingine unachokijali zaidi ya lengo lako kuu, basi jua kitu hicho kitakuwa kikwazo kwa lengo lako kuu.
Kila unaposema lakini hii ni muhimu zaidi katika kulinganisha na lengo lako kuu, jua unalifanya lengo hilo kuwa dogo na lisilo na umuhimu mkubwa.
Hatua ya kuchukua;
Inapokuja kwenye lengo lako kuu la maisha, hakuna kingine unachopaswa kukijali kuliko hilo.
Hilo ndiyo linapaswa kuwa namba moja na mengine yote yawe tayari kusubiri.
Tafakari;
Kinachopata nafasi ni kile chenye umuhimu zaidi, kinachojaliwa zaidi.
Kama hufanyii kazi lengo lako kuu ni kwa sababu hujalifanya kipaumbele cha kwanza kwenye maisha yako.
Kocha.