#SheriaYaLeo (144/366); Usiyaamini macho yako mara zote.
Wale wanaotaka kukushawishi kwa namna mbalimbali, huwa wanatumia zaidi picha ili kukujengea taswira ya aina fulani itakayokufanya uamini vitu fulani.
Wanajua udhaifu wetu binadamu kwamba kile tunachoona huwa kina nguvu kubwa na huwa tunakiamini zaidi.
Wanaunganisha picha mbalimbali pamoja na maelezo yanayotengeneza taswira ya aina fulani kwetu.
Halafu sisi wenyewe, kupitia kile tunachoona tunajenga imani ya aina fulani.
Kama unataka kuujua ukweli, usiamini macho yako mara zote.
Badala yake chagua kudadisi zaidi kile unachokiona.
Jiambie inawezekana ukweli siyo kile kinachoonyeshwa, na hapo utapata fursa ya kujua ukweli.
Kunapokuwa na tofauti kati ya kile watu wanachosikia na kile wanachoona huamini zaidi kile wanachoona.
Ndiyo maana taswira hutumika zaidi kwenye ushawishi wa hila kuliko maelezo.
Sheria ya leo; Watu wenye hila huwa ni wazuri sana kwenye maigizo. Wanajua kutumia picha na mwonekano kuficha nia zao halisi. Usiwe rahisi kuamini kile unachoona, badala yake dadisi kwa undani ili uweze kujua ukweli.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UdadisiUpekeeUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji