#SheriaYaLeo (160/366); Wavuruge wasijue nia yako halisi.

Kwa chochote unachotaka, kuna watu ambao ni kikwazo kwako, ambao wapo tayari kukuzuia usikipate.

Njia bora ya kuwavuka watu hao na kupata kile unachotaka ni kuwavuruga.
Unawavuruga kwa kuwahadaa, kuwafanya waone unataka kitu kingine ambacho siyo nia yako halisi.

Kwa njia hii huendei wazi lengo lako halisi, kitu ambacho kitawafanya watu wakuwekee vikwazo kirahisi.
Lakini pia huwi msiri, kitu ambacho kitafanya watu wakuchunguze zaidi.
Unakuwa muwazi kwa kisichokuwa sahihi na hivyo kuwapoteza wakati kwa ndani ukifanya kile unachotaka bila ya vikwazo vyovyote.

Kwa kufanya hivyo unanufaika na mambo matatu;

Kwanza utaonekana ni mtu rafiki na muwazi. Kwa sababu unayaweka mambo yako wazi, japo siyo halisi, watu watakuona ni muwazi na hivyo kukuamini zaidi.

Pili unaficha nia yako halisi hivyo hakuna anayeweza kuwa kikwazo kwako kwenye nia hiyo. Kwa kuwa kuna vitu vingine unavyoweka wazi zaidi, vile halisi havionekani.

Tatu unawapa maadui zako kitu cha kuhangaika nacho ambacho hakina madhara kwako ila kinawachosha wao. Kwa kuwa maadui zako watatafuta kitu cha kukushambulia nacho, unapowapa kitu kisichokuwa na madhara kwako, unapata nafasi ya kufanyia kazi kile kilicho sahihi bila ya mashambulizi kutoka kwa maadui.

Sheria ya leo; Waonyeshe maadui zako unataka kitu fulani ambacho siyo unachotaka kwa uhalisia. Wao watahangaika kukuzuia kwenye hicho unachoonyesha na hilo kukupa nafasi ya kufanyia kazi kile unachotaka kweli bila ya usumbufu.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji