#SheriaYaLeo (161/366); Wafanye watu wajisikie wako juu.

Watu wanapenda sifa na kutukuzwa, wanapenda kuona wapo juu na wengine wanawategemea kwa mambo mbalimbali.

Pale unapotaka kitu kutoka kwa watu, hasa wale wenye mamlaka, wafanye wajione wako juu.
Wafanye waone upo chini yao na unawategemea sana kwa kile unachotaka.
Hilo linawafanya wajione ni muhimu na kuwa tayari kukupa kile unachotaka.

Kuna ambao wanapenda umuhimu wao uonyeshwe hadharani ili wengine wajue.
Na kuna ambao hawapendi umuhimu wao kuonyeshwa hadharani.

Kila mtu anapenda kuonekana yupo juu, anapenda kuonekana ni wa muhimu.
Wape watu hayo na watakuwa tayari kukupa kile unachotaka.

Sheria ya leo; Unapaswa kujua ni kitu gani hasa ambacho watu wanataka. Ukishakijua, wapatie kwa namna wanavyotaka na wao watakuwa tayari kukupa kile unachotaka.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji