#SheriaYaLeo (162/366); Waambukize watu hisia chanya.
Sisi binadamu ni viumbe wa kihisia.
Unapokuwa ndani ya kundi lolote lile, hasa kama kiongozi, waambukize watu hisia chanya kwa kuwapa hamasa ya kuweza kufanya makubwa zaidi.
Washirikishe maono makubwa na malengo ya kufika kwenye maono hayo.
Waonyeshe ung’ang’anizi katika kufikia maono hayo.
Pia onyesha kujiamini kwenye kile kinachofanyiwa kazi.
Mara kwa mara badili mambo yaliyozoeleka na kujaribu vitu vipya na vyenye changamoto.
Haya yote yanawapa wengine hamasa kubwa kwenye kile kinachofanyika.
Yanawaondoa kwenye mazoea na kuwapa msukumo wa kufanya zaidi.
Yanawafanya waache kuridhika na mafanikio kidogo waliyopata badala yake kuyaendea mafanikio makubwa zaidi.
Muhimu zaidi ni kutokuwa na hofu na kupokea mawazo mapya, kitu kinachokuwa tiba kwa wengine.
Hilo linawafanya watu kuondoa hofu na kuweza kufikiri badala ya kufanya tu kwa mazoea.
Sheria ya leo; Watu wanashawishiwa zaidi na hisia za watu wengine. Tumia asili hiyo ya binadamu kuweza kuwashawishi kwa kutumia hisia chanya. Wape watu hamasa ya kuweza kufanya makubwa kuliko walivyozoea kufanya.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji