2664; Ni wewe umewafundisha.
Kama watu wanakuchukulia kwa namna ambayo hupendezwi nayo, wao siyo wa kulaumu, bali wewe ndiye wa kujilaumu.
Kwani kwa vyovyote vile watu wanavyokuchukulia, ni wewe umewafundisha.
Wewe ndiye umewaonyesha na kuwaruhusu kwa namna gani wanaweza kukuchukulia.
Kama watu wanakudharau, ni kwa sababu umewaonyesha ni sawa wao kukudharau.
Kumbuka kwenye maisha hupati kile unachostahili, bali unapata kile unachovumilia.
Matokeo unayoyapata ni kwa sababu ndiyo umeyavumilia hayo.
Kama ungekataa kwamba hayapo kwa viwango vyako, ungepata matokeo ya tofauti.
Hatua ya kuchukua;
Jiwekee viwango vyako kwenye kila eneo la maisha yako na usikubali chochote chini ya viwango hivyo.
Wafundishe watu namna sahihi ya kukuchukulia wewe, kwa kuonyesha wazi na kwa vitendo nini unaweza kuvumilia na nini huwezi.
Usitake kuwaridhisha watu kwa kuumia wewe.
Tafakari;
Ukiacha kuwalaumu watu kwa yale yanayotokea kwenye maisha yako na kujua yote chanzo ni wewe, utaweza kujenga aina ya maisha unayotataka.
Hakuna anayekuonea au kukudharau, yote hayo yanaanzia kwako kwenyewe.
Kocha.
Asante sana umeandika kwa hisia kweli ukurasa huu.
Chochote kinachotokea niliweka nafasi kwa watu wanione nilivyo na wanichukulie hivyo.
Hakuna anaekuumiza ni kwasababu ulichagua kuumizwa.Kuruhusu hisia zikutawale .
LikeLike
Kabisa,
Tukitambua hili, tutakuwa huru kabisa.
LikeLike