#SheriaYaLeo; (168/366); Dhibiti machaguo unayowapa watu.

Watu huwa wanapenda kuona wana uhuru wa kuchagua mambo yao wenyewe.

Lakini machaguo yanapokuwa mengi, huwa inakuwa vigumu kwa mtu kuweza kuchagua.
Anajikuta njia panda na kushindwa kuchagua kitu kimoja.

Ili kuwasaidia watu kufanya maamuzi na wewe kuweza kupata kile unachotaka, dhibiti machaguo unayowapa watu.

Wape machaguo machache, lakini yote yanakuwa na manufaa kwako.
Kwa kuwapa machaguo wanajiona wako huru kuchagua.
Lakini sasa, chochote wanachochagua kinakuwa na manufaa kwako.

Ukiwapa watu machaguo ya aina hii, hawaoni kama unawashurutisha, hivyo wanafanya kile unachotaka wafanye bila ya ubishi.

Kwa sababu watu hawana muda wa kuchimba kwa undani kujua ukweli wa mambo, hawatahangaika sana na machaguo yaliyopo, badala yake watafurahia kuwepo kwa uhuru wa kuchagua.

Ambacho hawatajua ni kwamba umedhibiti machaguo hayo na hivyo hawako huru kama wanavyodhani.

Sheria ya leo; Huwa kuna usemi; kama utaweza kumfanya ndege aingie kwenye kizimba mwenyewe, ataimba vizuri zaidi. Wape watu machaguo ambayo yote yana manufaa kwako, wataona wako huru kuchagua, ila chochote wanachochagua kinakunufaisha.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji