#SheriaYaLeo (171/366); Wafanye wengine waje kwako.

Pale unapoonekana kuwahitaji sana wengine na kwenda kuwafuata, unaishia kuonekana wa kawaida na hakuna anayekuthamini.

Lakini pale unapowafanya watu waje kwako, kwa kuwa siyo rahisi wewe kupatikana, unakuwa wa tofauti na unathaminika.

Kwa chochote unachofanya, wafanye watu waje kwako wakiwa na uhitaji.
Wafanye waje wa kuombe ufanye kitu kwa ajili yao.
Ni kwa njia hiyo ndiyo unapata mamlaka makubwa kwenye hicho unachofanya.

Epuka kuonekana wewe ndiye mwenye uhitaji zaidi kwa wengine.
Watu huwadharau wale wenye uhitaji mkubwa kwao na kuwaheshimu wale ambao wanawahitaji zaidi.

Sheria ya leo; Unahitaji hatua moja tu ya kuwafanya watu waje kwako wakiwa na uhitaji mkubwa wa kile unachofanya au ulichonacho. Hilo litawafanya wakutegemee na kukuthamini zaidi.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji