#SheriaYaLeo (182/366); Weka wazi mbinu zako.

Pamoja na kwamba ni muhimu kutumia mbinu mbalimbali kuficha nia yako halisi, kuna wakati utalazimika kuweka mbinu na nia yako wazi.

Pale watu wanapojua kwamba huwa unatumia mbinu mbalimbali kuficha nia yako, hilo linakosa nguvu.
Kwani inakuwa vigumu kwao kuendelea kukuamini.

Ni katika hali hiyo ndiyo unapaswa kuwa kuwazi, kuweka wazi mbinu na nia yako.

Cha kushangaza, watu watakuwa tayari kukupa ushirikiano licha ya kujua kabisa mbinu zako na nia uliyonayo, ambayo siyo nzuri kwao.

Pamoja na watu kujua kwamba unawadanganya, bado watakuwa tayari kukupa ushirikiano.
Maana watakuchukulia kama muongo anayeaminika badala ya wale wanaoficha uongo wao.

Kama ambavyo Kierkegaard amewahi kusema, dunia inapenda kudanganywa. Hivyo unapoweka wazi mbinu zako hupotezi watu, bali unawapata kwa wingi zaidi.

Na kama unawaambia watu kile wanachotaka kusikia, watakusikiliza hata kama wanajua unadanganya. Tena watakuamini zaidi pale unapoweka wazi mbinu na nia zako kuliko unapozificha.

Sheria ya leo; Pale ambapo huwezi tena kuficha mbinu na nia yako, weka wazi mambo yako. Bado utawapata wengi watakaokubaliana na wewe kwenye hali hiyo.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji