#SheriaYaLeo (195/366); Tumia vizuri utofauti.
Kuna utofauti ambao wewe unao ukilinganisha na watu wengine.
Unapaswa kutumia utofauti huo kuwafanya watu washawishike zaidi na wewe.
Na njia bora ya kufanya hivyo ni kuhakikisha mtu unayetaka kumshawishi anajua utofauti huo.
Kwanza unamweka kwenye hali ambayo anakosa kile ulichonacho.
Kisha unakuja kumpa hicho ulichonacho ambacho alikuwa amekosa.
Kwa namna hiyo unakuwa kama mkombozi kwake, maana umekuja kumpa kile ambacho anakuwa amekikosa.
Watu wakizoea sana kile unachowapa wanakichukulia kawaida na kuona hakina umuhimu mkubwa.
Unapowaweka kwenye hali ya kukosa kitu hicho, wanaona ni jinsi gani kilivyo adimu kupatikana na hivyo kukithamini zaidi.
Sheria ya leo; Tumia vizuri utofauti ulio nao. Unaweza kufanya hivyo kwa kuonyesha sifa bora na za tofauti ulizonazo na ambazo wengine hawana. Au chagua kundi ambalo tabia zako ni adimu na zitakufanya uwe wa kipekee.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji