#SheriaYaLeo (199/366); Watengenezee Majaribu.
Watu huwa hawataki majaribu, japo majaribu huwa ni sehemu ya maisha ya kila siku.
Watu wanachotaka ni kuyakubali majaribu, kwa sababu kuyakataa kunaleta msongo mkubwa kwao.
Ili kuwa na ushawishi kwa watu, watengenezee majaribu ambayo ni makubwa na hawawezi kuyahimili.
Majaribu hayo yanapaswa kuwalenga wao moja kwa moja ili yaweze kuwa na nguvu.
Majaribu unayowatengenezea watu yanapaswa kulenga udhaifu walionao.
Tambua kwamba kila mtu ana udhaifu wake mkuu ambapo ndipo madhaifu yake mengine yanachipukia.
Udhaifu wa mtu unaweza kuwa tamaa, ulafi, ulevi, uzinzi, uchoshi au kitu ambacho anakipenda sana ila amekuwa anakikosa.
Watu huwa wanaonyesha udhaifu wao kwenye mambo mbalimbali wanayofanya.
Inaweza kuwa kwenye tabia zao, mazungumzo yao, mavazi yao au mambo yanayowapa msongo.
Kwa kujua udhaifu mkuu wa mtu na kumtengenezea majaribu kwenye udhaifu huo, utanasa tamaa zao na kuwapa matumaini ya kupata raha kitu ambacho kitakuwa na ushawishi mkubwa kwao.
Ni rahisi kwa mtu kukubaliana na majaribu kuliko kuyapinga, hasa pale yanapokuwa yamelenga udhaifu mkuu walionao.
Sheria ya leo; Tafuta udhaifu mkuu ambao watu wanao kisha watengenezee majaribu kwenye udhaifu huo. Hilo litafanya uwe na ushawishi mkubwa kwa watu maana ni vigumu kwao kuyapinga majaribu yanayogusa madhaifu yao.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji