2699; Msimamo.
Kila mtu anajua kile anachopaswa kufanya ili kupata kile anachotaka.
Wengi huwanza mpaka kuchukua hatua hizo.
Lakini bado wengi hawafanikiwi.
Kwa sababu wanachokosa ni msimamo.
Hawafanyi jambo kwa kujirudia rudia kwa muda mrefu.
Wanapoona matokeo hayaji haraka kama wanavyotaka, wanaacha kufanya.
Msimamo kwenye ufanyaji ni moja ya mahitaji muhimu sana kwenye mafanikio.
Kukosa msimamo ni kikwazo kikubwa sana kwa mtu kufanikiwa.
Kwani haijalishi una sifa nyingine nzuri kiasi gani, bila msimamo kwenye ufanyaji sifa hizo zinakosa maana.
Napoleon aliwahi kusema ni bora kuwa na jenerali mmoja mjinga kuliko kuwa na majenerali wawili wenye akili sana.
Hiyo yote inakuja kwenye msimamo, jenerali mmoja hata kama atakuwa mjinga, atakuwa na msimamo kwenye huo ujinga wake.
Lakini majenerali wawili, hata wawe wajanja kiasi gani, itakuwa vigumu kuwa na msimamo mmoja, kila mara watakuwa wanavutana.
Hatua ya kuchukua;
Upo tayari kufanya kitu kwa muda mrefu kiasi gani hata kama hupati matokeo unayotegemea?
Hilo ndiyo linalotofautisha matokeo wanayopata watu.
Jijengee msimamo wa kufanya kwa muda mrefu bila kuchoka au kukata tamaa.
Na kwa hakika matokeo mazuri utayapata.
Tafakari;
Dunia inakuhadaa na njia za mkato za mafanikio.
Wakati mafanikio ya kweli yanatokana na msimamo wa kufanya kitu kwa muda mrefu bila kuchoka wala kukata tamaa.
Usihadaike na yale watu wanakimbizana nayo, simama kwenye kile kilicho sahihi.
#Let’sBuildBusinesses
#NothingElseMatters
#BillionairesInTraining
Asante Sana kocha, hakika nahitaji kusimamia msimamo wangu kuliko jambo lolote, neno langu na liwe sheria kwangu mwenyewe, hakika nahitaji msimamo ili kuzifikia ndoto zangu3,asante sana kocha.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike