#SheriaYaLeo (207/366); Cheza na utata.
Kunasa umakini wa watu na kuwafanya wakufuatilie, unapaswa kuonyesha sifa ambazo ni kinyume na mwonekano wako.
Unapaswa kutengeneza hali ya utata ambao unafanya watu washindwe kukuelewa.
Sisi binadamu huwa hatuwezi kutulia pale ambapo hatujakielewa kitu.
Huwa tunakifuatilia mpaka tukijue na kukielewa kwa undani.
Pale unapoonyesha utata, watu watakufuatilia ili wajue zaidi.
Ni katika kukufuatilia huko ndiyo unakuwa na ushawishi mkubwa kwao.
Fanya kitu ambacho ni tofauti kabisa na unavyoonekana.
Kama una sura ya upole onyesha hali ya ukatili.
Usihofie kwamba kile unachoonyesha kitaharibu sifa yako na kuifanya hasi.
Watu huwa wanavutiwa na kile wasichoelewa bila ya kujali ni kizuri au kibaya.
Na pia wema peke yake huwa hauna ushawishi mkubwa.
Sheria ya leo; Hakuna mtu ambaye kwa asili ni mtata na asiyeeleweka, hicho ni kitu ambacho unapaswa kukitengeneza na kukitumia kama njia ya kuwashawishi watu.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUwajibikajiUtegemeano