#SheriaYaLeo (208/366); Jua wakati sahihi wa kupotea.

Ili kuwa na ushawishi mkubwa kwa watu, hupaswi kupatikana wakati wote.
Kuna wakati unapaswa kupotea na usipatikane kabisa.

Pale watu wanapojua unapatikana muda wote wanakuchukulia poa, maana wanajua upo tu.

Lakini pale unapopotea, tena bila ya taarifa ndiyo watu wanashtuka kwa kuwa hawakutegemea hilo hivyo hawakuwa wamejiandaa.

Pale unapokuja kupatikana tena watu wanakupa umakini mkubwa kwa sababu hawajui ni wakati gani utapotea tena.
Hilo linawafanya watu washawishike zaidi na wewe.

Umakini, mapenzi na hata ushawishi huwa havifi kwa kukosekana, bali kwa kuwepo kupitiliza.
Pale kitu kinapopotea, watu ndiyo wanakipenda na kukithamini zaidi.

Sheria ya leo; Ni wakati ambao haupo ndiyo watu watakuthamini zaidi. Watasahau makosa yako na kusamehe madhambi yako. Pale utakaporudi watakukimbilia kwa shauku kubwa. Utaonekana kama vile umerudi kutoka kwenye kifo. Hilo litaongeza zaidi ushawishi wako.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji