2705; Imani na matendo.

Imani na matendo ni vitu vinavyokwenda pamoja.
Ni mapacha ambao hawawezi kutenganishwa.

Ili uweze kufanya makubwa zaidi kwenye maisha yako, ni vitu viwili unavyohitaji kwa pamoja.

Imani bila matendo ni mfu, hakuna chochote kitakachotokea kwa kuamini tu. Lazima mtu uchukue hatua kwenye kile unachoamini.

Matendo bila imani ni kujiweka kwenye kukata tamaa.
Kwani hakuna hatua chache utakazochukua na zikaleta matokeo makubwa.
Unahitaji imani ya kuendelea kufanya licha ya kutokuona matokeo kwa haraka.

Vitu hivyo viwili vikienda pamoja na kwa ukubwa, hakuna kinachoweza kukushinda.
Kama utakuwa na imani thabiti huku ukicgukua hatua kubwa kabisa, hakuna kinachoweza kukuzuia kupata mafanikio makubwa.

Hatua ya kuchukua;
Kuwa na imani thabiti na isiyoyumbishwa na chochote kisha chukua hatua kubwa zaidi ya ulivyozoea kuchukua.
Muunganiko huo una nguvu ya kukupa chochote unachotaka.

Tafakari;
Ukiwaangalia wale waliofanya makubwa kuliko wewe, utaona wengi siyo kwamba wana uwezo mkubwa sana.
Bali wana imani thabiti na wanachukua hatua kubwa.
Ukifanya hivyo hata wewe lazima utapata matokeo makubwa.

#Let’sBuildBusinesses
#NothingElseMatters
#BillionairesInTraining