#SheriaYaLeo (210/366); Tumia lugha ya picha.
Kuwasiliana na watu kwa njia ya kawaida, ambapo unatumia maneno pekee huwezi kuwa na ushawishi mkubwa.
Hiyo ni kwa sababu watu huwa wanayasahau maneno haraka.
Lakini unapowasiliana na watu kwa kutumia lugha ya picha, unakuwa na ushawishi mkubwa zaidi.
Hiyo ni kwa sababu watu huwa wanakumbuka picha kwa muda mrefu.
Yafanye maneno yako kuwa ya mafumbo na yasiyoeleweka na tumia zaidi vitendo wakati wa kuzungumza.
Onyesha hali ya mwendo kwa vitendo wakati unazungumza.
Onyesha kujiamini siyo kupitia maelezo bali kupitia rangi na picha.
Hata pale vyombo vya habari vinapokuandika, usiviache vikuandike kwa namna vinavyotaka.
Badala yake wape maigizo na vitu vinavyoonekana.
Vyombo vya habari huwa vinapenda sana mwonekano na maigizo na hivyo vitasambaza zaidi taarifa zako.
Usiwahutubie watu, hilo huwa halifanyi kazi.
Badala yake jifunze kutoa ujumbe wako kupitia picha na kugusa hisia.
Hapo watu watanaswa na kufuatilia kwa makini.
Kitu ambacho kinawafanya washawishike na unayowaambia.
Sheria ya leo; Weka umakini mkubwa kwenye njia unayotumia kutoa ujumbe wako kuliko ujumbe wenyewe. Picha huwa zina ushawishi zaidi kuliko maneno pekee. Hivyo ujumbe wako mkuu unapaswa kuwa kwa lugha ya picha.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUbunifuUdadisi
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji