2707; Mtu wa ajabu.

Jamii huwa inapenda kumwelewa kila mtu kwenye yale anayoyafanya.

Pale jamii inaposhindwa kumwelewa mtu, huwa inamchukulia ni mtu wa ajabu kabisa.

Inamwona ni mtu asiyefaa au aliyepotoka na ambaye hawezi kufanikiwa.

Anapopitia magumu ambayo kila mtu anayapitia, yeye ataonekana anayapitia hayo kwa sababu ya utofauti wake.

Wengi kwa kutokutaka kusumbuana na jamii, huwa wanaenda nayo kwa jinsi inavyokwenda.
Kwa kufanya yale wanayotegemewa kufanya.

Na hapo ndipo wanapoishia kupata matokeo ambayo wengine pia wanayapata.
Na ukishapata matokeo wanayoyapata wengine, hakuna namna unaweza kupata mafanikio makubwa.

Hivyo hilo linakuweka njia panda.
Uonekane wa kawaida kwenye jamii lakini usifanikiwe.
Au uonekane wa ajabu kwenye jamii ila upate mafanikio makubwa unayoyataka.

Ni lazima uchague kimoja, kwa makusudi au kwa kufuata mkumbo.

Hatua ya kuchukua;
Kubali kuonekana wa ajabu kwenye jamii ili uweze kupata kile unachokitaka.
Usihangaike sana kutetea kile ambacho jamii inakiona ni cha ajabu kwako.
Badala yake kazana kukifanyia kazi ili uzalishe matokeo ya tofauti.

Tafakari;
Kila kitu kipya ambacho kimeinufaisha dunia, mwanzo kilionekana cha ajabu na kisichowezekana.
Kila aliyeleta mabadiliko makubwa duniani, mwanzo alionekana wa ajabu na aliyechanganyikiwa.
Hilo halitakuwa tofauti kwako, lazima uwe tayari kulivuka ili kufanya makubwa

#Let’sBuildBusinesses
#NothingElseMatters
#BillionairesInTraining