#SheriaYaLeo (212/366); Raha ya maigizo.
Huwa tunayaangalia maigizo na kuyafurahia japo tunajua siyo kitu cha kweli.
Mavazi ya waigizaji na jinsi mtiririko unavyokwenda huwa inakamata sana hisia na umakini wetu.
Japo ni maigizo, huwa tunachukulia ni uhalisia.
Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye maisha halisi.
Ili kuweza kuwashawishi watu, unapaswa kuwa na maigizo.
Unapaswa kuwa na mwonekano na mavazi ambayo yatanasa umakini na hisia za watu.
Pale unapokutana na wale unaotaka kuwashawishi, mwonekano wako unawateka na hilo linarahisisha zaidi ushawishi wako.
Japo unakuwa unaigiza, wengine wanaamini na kuvutiwa na hilo.
Sheria ya leo; Kila unapokutana na wale unaotaka kuwashawishi, wape hisia za kuwa kwenye maigizo. Mwonekano unaokuwa nao unapaswa kuteka hisia na umakini wao ndiyo uweze kuwashawishi.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji