#SheriaYaLeo (216/366); Wazungumzie wao na kuwasifia.
Huwa tunajaribu kuwashawishi watu kwa kueleza sifa zetu na makubwa ambayo tumeyafanya.
Tunaahidi makubwa zaidi ambayo tunakwenda kuyafanya.
Na pia tunaomba wengine watusaidie kwa namna mbalimbali.
Tunachosahau ni kwamba kufanya yote hayo tunakuwa tumeweka umakini wote kwetu wenyewe.
Kwenye dunia ambayo kila mtu anajifikiria zaidi yeye mwenyewe, hilo linawafanya watu waache kutusikiliza na kufikiria mambo yao wenyewe.
Hilo linafanya ushawishi kwao kuwa mgumu zaidi.
Njia bora ya kuwashawishi watu ni kuweka umakini wako kwao na siyo kwako.
Badala ya kujingelea kuhusu wewe mwenyewe, waache wao wajiongelee wenyewe.
Waache wao wawe ndiyo vinara wa mazungumzo kwa kuwapa nafasi ya kujieleza zaidi.
Wafanye waone maoni yao ni bora zaidi na kile wanachosimamia ndiyo msingi sahihi.
Umakini wa hali hiyo ni adimu sana kwenye zama hizi na watu wana kiu kubwa ya kuupata.
Kwa kuwapa watu umakini huo, wanaondoa mapingamizi yao na hivyo kuwa rahisi kushawishika na wewe.
Sheria ya leo; Kwenye mazungumzo, jaribu kuwafanya wengine wafanye asilimia 70 ya uongeaji bila ya wao kujua. Wape nafasi kubwa ya kujiongelea zaidi wao wenyewe na itakuwa rahisi sana kuwashawishi.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji