#SheriaYaLeo (217/366); Tumia hisia kali.

Pale unapotaka kuonyesha msisitizo wa kitu na kuwa na ushawishi mkubwa, unapaswa kutumia hisia kali.

Hisia kali, hasa za chuki huwa zinaeleweka sana na kuwashawishi wengine.

Hiyo ni kwa sababu zinakuwa ni hisia walizonazo ila hawathubutu kuziweka wazi.

Hivyo pale wewe unapoziweka wazi, wanakuona kama mwakilishi wao na kushawishika na wewe.

Onyesha kile ambacho wengine wanahofia kukionyesha, sema kile wanachotaka kusema ila wanashindwa.
Hayo yatawafanya waone mamlaka makubwa ndani yako na wawe tayari kushawishika na wewe.

Sheria ya leo; Jifunze jinsi ya kutumia hisia kali kuwashawishi wengine kwa kuonyesha kile wanachotaka kuonyesha ila hawathubutu. Hakuna kitu chenye ushawishi kama hisia kali zinapotumika vizuri.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji