#SheriaYaLeo (220/366); Zingatia maslahi yao binafsi.
Njia ya haraka na ya uhakika ya kuteka akili za watu na kuwashawishi ni kuwaonyesha jinsi ambavyo kitu kinakwenda kuwanufaisha wao wenyewe.
Maslahi binafsi ndiyo nguvu yenye msukumo mkubwa kwa wengi.
Tukio muhimu linaweza kuwahamasisha watu mwanzoni.
Lakini baada ya hamasa hiyo ya mwanzo kutulia, kitakachowabakisha watu kwenyw hilo ni manufaa yao binafsi.
Watu hawawezi kubaki kwenye kitu kama hakuna manufaa binafai wanayoyapata.
Manufaa binafsi ndiyo msingi imara unaowanasa watu na kuwafanya wabaki kwenye kitu kwa muda mrefu.
Tukio linaweza kuwahamasisha watu, lakini ni manufaa binafsi ndiyo yatawabakisha watu kwenye kitu hicho.
Sheria ya leo; Waonyeshe watu ni manufaa gani yaliyopo kwa ajili yao na watashawishika zaidi.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji