#SheriaYaLeo (223/366); Nasa Ufahari wao.

Kila mtu huwa ana ufahari au majigambo ndani yake. Hali ya kujiona ni muhimu kwenye hii dunia.
Pale mtu anapokushambulia na hujui ni kwa nini, mara nyinyi ni kwa sababu unakuwa umetishia ufahari wao.

Mara zote unapaswa kuhakikisha watu wanajisikia vizuri kuhusu wao wenyewe kwa kuchochea ufahari wao.
Unaweza kutumia njia mbalimbali kama kuwasifia, kuwapa zawadi, kuwasaidia au kuonyesha wamekuwa na msaada mkubwa kwako.

Hayo yote yatanasa ufahari wao na kuwafanya wajione ni wa muhimu kabisa, kitu kitakachowafanya wakusikilize na kushawishika na wewe.
Unaondoa ile hali ya wao kujilinda na kujitetea, badala yake wanakuamini na kujisikia vizuri kwa uwepo wako kitu kinachowafanya washawishike zaidi na wewe.

Tumia vizuri ufahari wa watu katika kuwafanya washawishike zaidi na wewe.

Sheria ya leo; Pale watu wanapojiona wakiwa salama, pale unaponasa ufahari wao, wanaacha kujilinda na kujitetea na kuwa rahisi kushawishika.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji