#SheriaYaLeo (227/366); Waachie watu hisia.
Watu wengi huwa wanakazana kutumia maneno kuwashawishi watu.
Iwe ni kupitia mazungumzo au maandiko.
Wanasema mengi wakiamini baadhi yatakuwa na ushawishi kwa watu hao.
Lakini maneno matupu huwa hayana ushawishi mkubwa.
Badala yake yanawaacha watu wakiwa na wasiwasi.
Kwa sababu watu wanaweza kuondoka na maana tofauti na uliyokusudia.
Kuna njia moja ya uhakika ya kuwashawishi watu ambayo ni kuwaachia hisia.
Kwa njia hiyo, unawaacha watu wakiwa na hisia nzuri kuhusu wewe.
Kwa kuwa watu huwa wanafanya maamuzi kwa hisia, pale unapogusa hisia za watu, unakuwa na ushawishi mkubwa kwao.
Unapozungumza na watu, iwe ni ana kwa ana, mawasiliano au hotuba, usitumie maneno matupu pekee.
Badala yake tafuta kugusa hisia zao.
Tumia maneno na vitendo ambavyo vitagusa hisia zao.
Wafanye wajione ni wa kipekee na unawapenda na kuwajali sana.
Wafanye wajisikie kwamba utaendelea kuwa nao kwa muda mrefu.
Wafanye waamini kwamba umejitoa hasa kwa ajili yao.
Hisia hizo zinaondoa ile hali ya wasiwasi ambayo watu wanakuwa nayo na hivyo kuweza kushawishika zaidi.
Sheria ya leo; Fikiria unawaachaje watu baada ya kuwa umekutana nao. Fikiria kuwaacha wakiwa na hisia nzuri kuhusu wewe, hisia zinazowafanya wategemee mengi zaidi kutoka kwako. Hilo litawafanya washawishike zaidi na wewe.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji