#SheriaYaLeo (230/366); Tumia utani kushawishi.

Mabishano ni sumu kubwa kwenye ushawishi.
Ukishaingia kwenye ubishani unaishia kutengeneza adui na hivyo inakuwa vigumu kumshawishi mtu.

Ipo njia bora ya kuwashawishi watu ambayo ni kutumia utani.
Pale watu wanapotoa shutuma kuhusu wewe, badala ya kuanza kwa kuwashambulia, unaanza na utani kwanza.

Utani huo utawafanya watu wacheke.
Wakati wanacheka ndiyo unajibu shutuma hizo kwa namna ambayo inakuwa na ushawishi kwa watu.

Kucheka huwa kunawaweka watu kwenye hali ya kujisikia vizuri kitu kinachowafanya washawishike kirahisi.

Haijalishi watu wamekushutumu na nini, usijibu kwa hasira au ubishani.
Badala yake anza kwa utani ambao utawafanya watu wacheke, kisha jibu shutuma hizi kwa namna ambapo utakuwa na ushawishi mkubwa.

Sheria ya leo; Utani huwa una nguvu kubwa ya kuwashawishi watu. Unapotumia utani na watu kucheka, wanakuwa wamekaa upande wako na inakuwa rahisi kuwashawishi.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji