2728; Ni wewe umewafundisha.

Kwa namna yoyote ile ambayo watu wanakuchukulia, ni wewe mwenyewe umewafundisha wakuchukulie hivyo.

Umewapa ruhusa kwamba wanaweza kukuchukulia kwa namna wanavyokuchukulia.

Kama watu wanakudharau maana yake umewafundisha wakudharau. Kuna namna umejiweka ambayo inawafanya watu waone ni sawa kukudharau.

Kadhalika kama watu wanakuheshimu maana yake umewafundisha hivyo. Umejiweka kwa namna ambayo wanalazimika kukuheshimu.

Kila kitu unachojifanyia wewe mwenyewe, unawafundisha na kuwaruhusu wengine nao wakufanyie pia.

Kama unajiheshimu wewe mwenyewe, wengine nao watakuheshimu.
Na kama unajidharau wewe mwenyewe, ndivyo wengine watakavyokuchukulia pia.

Huna wa kumlaumu kwa namna wengine wanavyokuchukulia isipokuwa wewe mwenyewe.

Hatua ya kuchukua;
Ni kitu gani ambacho watu huwa wanakufanyia na hukipendi?
Jua ni wewe mwenyewe umewafundisha hivyo na ipo kwenye uwezo wako kubadili hilo.
Anza kujichukulia kwa namna ambavyo unataka watu wa kuchukulia na hivyo ndivyo watakavyofanya.

Tafakari;
Kwenye maisha hupati kile unachostahili, bali unapata kile unachovumilia.
Kuwa makini sana na mambo unayoyavumilia, kwani unawafundisha watu jinsi ya kukuchukulia.
Kama kuna chochote ambacho hutaki watu wakufanyie basi usijifanyie mwenyewe na usikivumilie pale yeyote anapokifanya kwako.

#Let’sBuildBusinesses
#NothingElseMatters
#BillionairesInTraining