#SheriaYaLeo (232/366); Wape ushindi kwenye mambo madogo.

Kama unataka kuwashawishi watu wakubaliane na wewe kwenye jambo kubwa unalotaka, wape kwanza ushindi kwenye mambo madogo.

Angalia mambo madogo ambayo hayana athari kwenye lile kubwa unalotaka, kisha kubaliana nao kwenye mambo hayo.

Katika kukubaliana nao kwenye mambo hayo madogo unakuwa umewaweka kwenye mtego wa kukubaliana na jambo lako kubwa unalolitaka.

Kila mtu anapenda ushindi, haijalishi ni mdogo kiasi gani.
Wape watu ushindi kwenye mambo madogo ili uweze kupata ushindi kwenye jambo kubwa kabisa.

Sheria ya leo; Jifunze kuondoa kujihami kwa watu kwa kukubaliana nao kwenye mambo madogo na yasiyokuwa na madhara kwenye kile unachotaka. Hilo litakupa ushawishi mkubwa kwao waweze kukubaliana na wewe kwenye jambo kubwa unalolitaka.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji