#SheriaYaLeo (233/366); Jinsi ya kuwakabili wasumbufu.
Kwenye maisha utakutana na watu wasumbufu.
Watu ambao kwa kuwa wana uwezo mkubwa kuliko wengine, huona kama hawahitaji kufuata taratibu wanazozifuata wengine.
Watu hao hufanya tofauti na wanavyofanya wengine na wanapoulizwa huomba radhi na kuahidi kufanya kwa usahihi.
Lakini bado wakati mwingine hawafanyi kwa usahihi, wanarudia makosa yale yale.
Haijalishi utaongea na watu hao kiasi gani, huwezi kuwashawishi kubadilika. Kwani huwa wanafanya hivyo makusudi kuonyesha utofauti wao.
Njia ya kukabiliana na watu wa aina hiyo na kuwashawishi kubadilika ni kuwapa kwa wingi kile wanachotaka.
Kwa kuwa watu hao wana uwezo mkubwa, huwa wanataka waheshimiwe. Basi hapo unawaonyesha heshima kupitiliza.
Kitendo cha kufanya hivyo kitawafanya wajisikie vibaya na kubadilika ili hali kama hiyo isijirudie tena.
Unapokutana na mtu msumbufu, ambaye anatumia uwezo wake mkubwa na wa tofauti kwenda kinyume na taratibu, usimlaumu kwa kufanya hivyo, bali mtukuze kwa kupitiliza.
Hilo litamkera na hivyo kuchagua kubadilika ili lisijirudie tena.
Sheria ya leo; Njia ya kuwakabili wasumbufu ni kuwaonjesha ladha ya dawa yao wenyewe, kuwapa kwa kupitiliza kile wanachotaka kupata kwa sababu ya uwezo wao mkubwa na utofauti wao. Kwa kufanya hivyo wanajisikia vibaya na kuamua kubadilika.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji