#SheriaYaLeo (234/366); Mhamasishaji mkuu.
Watu wengi huwa wanapenda kuhamasisha kwa kutumia maneno.
Lakini maneno pekee huwa hayana nguvu ya ushawishi.
Na pia huwa yanasahaulika haraka.
Kama unataka kuwa na ushawishi mkubwa kwa wengine, kuna mambo mawili muhimu unapaswa kuyazingatia.
La kwanza ni kuonyesha kwa vitendo. Watu wanaelewa, kuhamasika na kukumbuka zaidi vitu wanavyoona kuliko tu vile wanavyosikia.
La pili ni kugusa hisia zao. Watu huwa wanaelewa, kuhamasika na kukumbuka zaidi vitu ambavyo vinagusa hisia zao.
Chochote unachotaka kuwashawishi watu, usitumie tu maneno, badala yake onyesha kwa vitendo au mifano ya picha na hakikisha unagusa hisia zao.
Hata kama inabidi utumie maneno kuwaeleza watu, waweke kwanza kwenye hali ya kihisia na hiyo itafungua mioyo wao na kuwawezesha kuelewa na kuhamasika na kile unachowaambia.
Sheria ya leo; Kuwahamasisha watu ni sanaa. Unapaswa kutumia vitendo na kugusa hisia zao. Kwa kuwachochea kihisia, inakuwa rahisi kuingia kwenye mioyo yao na kuwahamasisha.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji