2731; Fanya kazi kwa juhudi na utafanikiwa.
Ipo nukuu moja ya Kiingereza ambayo ilikuwa ikitumiwa na moja ya familia tajiri sana dunian.
Nukuu hiyo kwa Kiingereza inasema; Work hard and you will succeed.
Ikimaanisha; Fanya kazi kwa juhudi na utafanikiwa.
Iko wazi na inaeleweka kabisa, kwamba ukifanya kazi kwa juhudi, lazima ufanikiwe.
Siyo labda utaweza kufanikiwa, bali ni lazima.
Hivyo kama unayataka mafanikio, wajibu wako mkubwa ni mmoja, weka juhudi kwenye kazi.
Jitume na kujisukuma zaidi kwenye kile unachofanya.
Nenda hatua ya ziada.
Na pale unapodhani kwamba unafanya kazi kwa juhudi, ongeza juhudi zaidi.
Haijalishi umekwenda kiasi gani, mara zote kuwa tayari kwenda hatua ya ziada.
Hakuna juhudi unayoweka ikapotea.
Hata kama huyaoni matokeo ya juhudi sasa, usikate tamaa na kuacha.
Wewe endelea kuweka juhudi, ukijua ni kanuni isiyoshindwa kwamba ukifanya kazi kwa juhudi lazima ufanikiwe.
Kama hautajifunza kitu kingine chochote kwenye maisha yako, hiki kimoja kitakusaidia sana.
Fanya kazi kwa juhudi na utafanikiwa.
Simama humo mara zote na utaweza kuleta mapinduzi makubwa kwenye maisha yako.
Hatua ya kuchukua;
Angalia ni juhudi kiasi gani unaweka kwenye kazi au biashara yako kwa sasa, kisha nenda kaongeze juhudi hizo zaidi.
Haijalishi unaweka juhudi kiasi gani, bado unaweza kuongeza juhudi zaidi.
Usibweteke, kila wakati weka juhudi kubwa zaidi.
Tafakari;
Fanya kazi kwa juhudi na utafanikiwa.
Jikumbushe hili kila siku na likusukume kwenda kuweka juhudi zaidi kwenye chochote unachofanya.
Uzuri wa kazi ni kwamba ipo ndani ya udhibiti wako.
Ni wewe unayeamua uweke juhudi kiasi gani kwenye kile unachofanya.
Hivyo mara zote weka juhudi za juu zaidi.
#Let’sBuildBusinesses
#NothingElseMatters
#BillionairesInTraining