#SheriaYaLeo (238/366); Tengeneza jicho la tatu.
Watu wengi huwa wamekwama kwenye wakati uliopo, kwa kuvurugwa na yale yanayoendelea kwenye wakati huo.
Wanayafikiria zaidi mambo hayo kitu kinachowapelekea kupata taharuki na kufanya maamuzi ambayo siyo bora sana.
Wanashindwa kuona zaidi ya kile kilichopo sasa au mbadala wake.
Wachache ambao wanaweza kufikiri zaidi ya kile kinachoendelea sasa huwa wanatumia uwezo mkubwa wa maono ulio ndani yetu binadamu.
Wanatumia jicho la tatu kuona zaidi ya kile kilichopo kwa wakati huo.
Ni maono hayo makubwa ndiyo yanayowatofautisha na wengine na kuwafanya wengi washawishike kuwafuata.
Maono makubwa ya baadaye ndiyo yanayowajenga viongozi wenye ushawishi mkubwa kwa wengine na hivyo kuwa na wafuasi wengi.
Sheria ya leo; Jenga nguvu ya mamlaka kwa kuonyesha uwezo wa kusoma mambo yajayo. Hiyo ni nguvu unayoweza kuijenga na ikakupa ushawishi mkubwa kwa wengine.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji