#SheriaYaLeo (241/366); Wajengee Kujiamini.

Unapojaribu kuwashawishi watu kwenye kitu chochote, moja kati ya haya matatu litatokea.

Moja unaweza kukosoa na kupinga maoni yao. Kitu ambacho kitawafanya wayalinde na kutatetea maoni yao na hapo watakuwa wagumu kushawishika.

Mbili unaweza usiguse kabisa maoni yao, usiyapinge wala kuyaunga mkono, kitu ambacho hakigusi hisia zao.

Tatu unaweza kuunga mkono maoni yao kitu ambacho kitagusa sana hisia zao, kukuona wewe ukiwa kama wao na wakashawishika zaidi na wewe.

Hakuna kitu ambacho watu wanapenda kama maoni yao kukubalika na watu wengine.

Watu huwa wanajiamini na kujikubali pale maoni yao yanapokubalika na watu wengine.
Hilo linarahisisha sana ushawishi wetu kwa watu wengine, kwa kuanza na kukubali maoni yao, unavunja kabisa upinzani wao.

Sheria ya leo; Jukumu lako kwa wengine ni rahisi, wajengee hali ya kujiamini na kukubaliana na maoni yao. Onyesha kujali mambo yao na kuheshimu maoni yao. Hilo litawafanya waone upo upande wao na hivyo kushawishika zaidi na wewe.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji