#SheriaYaLeo (243/366); Wachukulie kwa mtazamo sahihi.
Jinsi unavyowachukulia watu, ndivyo pia wanavyokuwa.
Matarajio uliyonayo kwa watu ndiyo matokeo utakayoyapata hata kama hutawaambia moja kwa moja.
Tegemea watu watafanya vizuri au kuwa vizuri na hilo ndiyo litatokea. Na kama utategemea watu wafanye vibaya au kuwa wabaya ndivyo watakavyokuwa.
Matarajio yetu kwa wengine huwa ndiyo utabiri ambao unatimia.
Hivyo ili uweze kuwashawishi watu, anza kwa kuwa na matarajio sahihi kwao.
Ni matarajio uliyonayo juu ya watu ndiyo yanakuwa uhalisia.
Kuwa na matarajio ya kile unachotaka kwa wengine na itakuwa rahisi kuwashawishi kwa namna unavyotaka.
Sheria ya leo; Kama kuna mtu unayetaka kumshawishi au kumwomba kitu, kuwa na matarajio kwamba ni mtu anayejali na atakayekubali. Kwa matarajio hayo utaongeza zaidi ushawishi kwake.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji