#SheriaYaLeo (244/366); Yatambue maoni yako mwenyewe.

Tambua ya kwamba hata wewe una maoni yako mwenyewe.
Tambua jinsi maoni hayo yanafanya kazi ndani yako.

Kubali kwamba haupo huru kama unavyodhani.
Umekuwa unashawishiwa na wengine kwa namna mbalimbali.

Lazima pia utambue ya kwamba siyo mjanja kama unavyojichukulia.
Unaweza kulaghaiwa na kushawishiwa kwenye vitu ambavyo hata havina umuhimu kwako.

Kwa kuyatambua haya, utaweza kuepuka ulaghai wa wengine ambao hupenda kutumia hali ya kutokujiamini ya watu ili kuwashawishi.
Kwa kuyajua madhaifu yako unawazuia wengine wasiweze kuyatumia kwa manufaa yao.

Sheria ya leo; Weka juhudi kwenye kuhakikisha unakuwa huru kweli huku ukijali maslahi ya wengine ili kuacha kuwategemea wengine na uepuke kulaghaiwa kwa sababu ya matarajio yako.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji