#SheriaYaLeo (249/366); Kuwa na machaguo mengi.

Ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kupata ushindi kwenye pambano lolote lile, unachohitaji siyo mkakati bora unaofuatwa hatua kwa hatua, bali mkakati wako unapaswa kuwa na machaguo mengi kuliko aliyonayo adui yako.

Badala ya kuwa na chaguo moja sahihi ambalo ndiyo unalikumbatia, mkakati bora ni kuwa na machaguo mengi ambayo yanakupa uwanja mpana zaidi.
Mkakati huo unakupa wewe nguvu zaidi ya kupambana na kuweza kuwashinda maadui.

Kwa kuwa na machaguo mengi unakuwa na nguvu kubwa ya kuwashinda maadui ambao wana machaguo machache.

Sheria ya leo; Ondokana na uongo kwamba mkakati sahihi ni kuwa na njia moja bora. Badala yake jua kuwa na machaguo mengi kuna manufaa makubwa zaidi. Waepuke sana wale wanaojinadi kumiliki kanuni ya siri kuu ya mafanikio na mamlaka. Kuwa na machaguo mengi ndiyo hitaji la msingi kabisa kupata ushindi.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji